Lebanoni kuchunga miili nane

Lebanoni
Image caption Bendera ya taifa la Lebanoni

Jeshi la Lebanoni linasema imepata mabaki ya watu nane wanaodhaniwa kuwa askari waliowahi kutekwa nyara miaka mitatu iliyopita na kundi la wanamgambo wa kiislam IS karibu na mpaka wake na nchi ya Syria.

Tangazo hilo limekuja saa kadhaa baada ya jeshi nchini humo kutangaza kusitisha shughuli zake dhidi ya kundi hilo la IS kwa lengo la kubadilishana taarifa juu ya askari waliokuwa hawajulikani walipo.

Mkuu wa usalama wa Lebanoni Abbas Ibrahim amearifu kwamba vipimo vya kuhakiki vinasaba vitafanywa ili kuwatambua na hivyo baadaye utafutaji wa mwili wa tisa utafanywa .

Mara baada ya serikali ya Lebanoni kuamua hatma ya askari wake, askari wa wanamgambo hao wa kiislam wataruhusiwa kuondoka eneo la karibu na mpaka wa Lebanoni.

Awali , wapiganaji wa jeshi la Lebanoni wa Hezbollah, ambao walianza kuwashutumu wapiganaji wa kikundi cha IS, nao wametangaza kusistisha mapambano.