Mahakama ya Guatemala yatengua uamuzi wa rais

Guatemala
Image caption Mwanasheria Ivan Velasquez aliyetaka kutimuliwa Guatemala

Mahakama ya Katiba ya Guatemala imesitisha uamuzi ulitolewa na raisi Jimmy Morales Kumfukuza mkuu wa ujumbe wa kupambana na rushwa wa Umoja wa Mataifa nchini humo, ambaye aliitisha uchunguzi ufanywe dhidi ya madai ya matumizi mabaya ya fedha katika kampeni za uchaguzi wa 2015.

Katika mkanda wa video uliosambazwa katika mitandao ya kijamii nchini Guatemala anaonekana rais Morales akitangaza kuwa Ivan Velasquez mwanasheria mwenye asili ya Colombia , na kumwita mtu asiyenanidhamu huku akimtaka aondoke nchini humo mara moja.

Rais Morales ni muigizaji wa zamani ambaye awali hakuwahi kushika ofisi za umma. Aliwastaajabisha wanasiasa nchini mwake baada ya kushinda nafasi ya uraisi kwa ahadi ya kupambana na rushwa pamoja na kutojali nchini Guatemala.