Liverpool yaichapa kichapo kizito Arsenal

Anfield
Image caption Majogoo wa Anfield Liverpool wakifurahia ushindi

Majogoo wa Anfield Liverpool wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kuichapa Arsenal mabao 4-0.

Mbrazil Roberto Firmino alianza kuipatia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 17, katika dakika ya 40 Sadio Mane akaongeza bao la pili.

Katika kipindi cha pili Mohamed Salah akawamsha tena mashabiki wa liverpool kwa bao la tatu kisha Daniel Sturridge akahitimisha kazi kwa bao la nne.

Bingwa mtetezi Chelsea walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Evertoni kwa mabao ya Cesc Fabregas ,Alvaro Morata, Stoke City wakatosha nguvu na West Bromwich Albion.

Tottenham Hotspur wakashindwa utumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kukubali sare ya bao 1-1 na Burnley