Sheria ya kutetea wanyama yapitishwa Lebanoni

Lebanon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Lebanon Michel Aoun

Kwa mara ya kwanza Lebanoni imekubali sheria ya kwanza ya kulinda ustawi wa wanyama. Rais Michel Aoun ametia saini muswada kuwa sheria baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura mapema mwezi huu.

Pendekezo la sheria hiyo limedumu kwa miaka kadhaa kabla ya kuwa sheria kamili ili kutunga na sheria za ustawi wa wanyama pamoja na kanuni za bustani za wanyama na maeneo mengine ambapo wanyama huhifadhiwa.

Pia inasema kuwa milki ya pori au ya hatari katika jaribio la kusitisha biashara yenye faida kutokana na wanyama hao.

Kikundi cha kutetea haki za wanyama kimeipokea sheria hiyo na kusema kwamba ni hatua kubwa na ya maendeleo iliyopigwa na kuahidi kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo inatimizwa .