Kerber atupwa nje mashindano ya Us Open

Naomi Osaka Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Naomi Osaka

Bingwa mtetezi wa michuano ya wazi ya tetesi ya Marekani Angelique Kerber ametupwa nje ya michuano hiyo na kinda wa Naomi Osaka.

Kerber anayeshika nafasi ya sita kwa ubora wa viwango kwa wanawake alipoteza kwa seti mbili ya 6-3 na 6-1 mchezo uliochezwa katika dimba la Flushing Meadows.

Kumpoteza mchezo kwa nyota huyo ni mwendelezo mbaya kwa mwaka huu baada ya kuondolewa kwenye raundi kwanza katika michuano ya wazi ya Ufaransa mapema mwaka huu.

Naomi Osaka raia wa japani mwenye umri wa miaka 19 anashikilia nafasi ya mia saba na tisini na nane kwa ubora wa viwango vya mchezo huo.