Wamasai wakataa kuondoka katika ardhi ya Serengeti Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Wamasai wakataa kuondoka katika ardhi ya Serengeti Tanzania

Mgogoro wa ardhi wilayani Loliondo, Kaskazini mwa Tanzania umeendelea kukua baada ya mamlaka za uhifadhi wilayani humo kuendelea kuchoma nyumba za watu wa jamii ya Kimaasai. Viongozi wa kijiji wa eneo hilo wameiambia BBC kwamba zaidi ya familia 500 zimeachwa bila makazi.

Wakati serikali ikisisitiza kwamba zoezi la kuwaondoa watu karibu na hifadhi ya Serengeti lazima liendelee, jamii ya Wamaasaia wa eneo hilo wameiambia BBC kwamba wako tayari kutoa uhai wao wakiilinda ardhi yao.

Mwandishi wetu Sammy Awami alitembelea eneo hilo na kutuandalia taarifa ifuatayo.