Wanaume wawili wakamatwa Zambia 'wakifanya mapenzi'

Mapenzi ya jinsia moja nchini Zambia ni kinyume cha sheria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapenzi ya jinsia moja nchini Zambia ni kinyume cha sheria

Polisi nchini Zambia wamewakamata wanaume wawili ambao "inadaiwa walipatikana wakifanya ngono", hiyo ni kwa mjibu wa gazeti linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo Times of Zambia.

Watu hao wawili mmoja akiwa na umri wa miaka 38 na mwingine miaka 30 - waligunduliwa ndani ya chumba moja ya malazi katika eneo la Kapiri, mji ulioko katika jimbo la kati nchini Zambia, Gazeti hilo linasema.

Msemaji wa polisi Diamond Likashi, amesema kuwa wanaume hao wawili kwa sasa wanazuiliwa na polisi wakisubiri mashtaka dhidi yao. Akiongeza kusema kuwa:

''Tunaendelea na uchunguzi wetu, ili tuweze kuthibitisha kesi hiyo mahakamani."

Lakini Dkt Mannasseh Phiri, ambaye mkereketwa wa kiafya, ameiambia BBC kuwa, Zambia inafaa kupigia msasa sheria ya mapenzi ya jinsia moja:

"Hakuna sheria nchini Zambia inayoharamisha tendo la mapenzi ya jinsia moja''.

''Sheria iliyopo, ambayo tuliachiwa na wakoloni walioitawala Zambia, ambao wenyewetayari wamepitishia ndoa ya jinsia moja, inaumzia uwezo wa kufanya tendo la ngono katika sehemu ambayo ni kinyume na kawaida yake.'' alisema mkereketwa huyo, huku akingeza kuwa, tumewasikia watu wakilaumiwa kuwa ni wapenzi wa jinsia moja, lakini wameachiwa huru, kwa sababu ni vigumu mno kuthibitisha."

Image caption Wanaume wawwili wakibusiana

Zambia - ambalo ni taifa la jamii kihafidhina na taifa la Kikristo kwa mjibu wa katiba ya nchi- linapinga kabisa ndoa au mapenxzi ya jinsia moja.

Sheria nchini Zambia inasema kuwa, mtu yeyoye akipatikana na kosa la ''kutenda tendo la ngono katika sehemu ambayo ni kinyume na kawaida yake'' anaweza kuhukumiwa jela kifungo cha hadi miaka 15.