Watawa bandia wajaribu kuiba kwenye benki Marekani

Picha ya washukiwa wawili Haki miliki ya picha FBI
Image caption Wanawake hao waliondoka bila kuiba chochote

Maafisa wa uchunguzi wa jinai nchini Marekani, FBI, wanawatafuta wanawake wawili ambao walijaribu kuiba pesa kutoka kwenye benki moja jimbo la Pennsylvania wakiwa wamevalia kama watawa.

Mmoja wa wanawake hao alichomoa bunduki na kuwaamrisha makarani wampe pesa wakati wa kisa hicho katika mji wa Tannersville.

Wote wawili walikuwa wamevalia mavazi ya watawa na mmoja alikuwa amevalia miwani.

Wanadaiwa kukimbia na kutoroka baada ya mmoja wa makarani wa benki kufungulia king'ora.

Haki miliki ya picha FBI
Image caption Mmoja wa wanawake hao alichomoa bunduki

Mada zinazohusiana