Ala ya muziki inayonogesha muziki wa mwambao Afrika Mashariki

Ala ya muziki inayonogesha muziki wa mwambao Afrika Mashariki

Je wafahamu muziki wa mwambao ni maarufu katika Pwani ya Afrika mashariki, kutokana na vionjo vyake ambavyo huleta ladha na nakshi ya aina yake katika muziki huo.

Kifaa cha muziki kijulikanacho kama Khanoon hunogesha zaidi muziki wa miondoko hiyo.

Nasoro Amour almaarufu kama Chollo Khanoon ni miongoni mwa wanamuziki wa mwanzo kujifunza ala hiyo asilia, ambayo kwa sasa ni watu wachache wanaoimudu.

Mwandishi wa BBC Munira Hussein alisafiri mpaka visiwani Zanzibar na kufanya mahojiano na mtaalamu wa ala hiyo ya muziki.