Jaribio la Korea ya Kaskazini lajadiliwa

Marekani
Image caption Rais wa Marekani Donald Trump

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amemwambia waziri wa mambo ya nchi nje wa Marekani, Rex Tillerson, kwamba uimarishwaji wa vikwazo dhidi ya Korea ya Kaskazini unaweza kuzaa matunda.

Taarifa iliyochapishwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi inaeleza kuwa mawaziri hao wawili walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu vikali jaribio la hivi karibuni la kombora la Pyongyang.

Lakini, taarifa hiyo inasema, Bw Lavrov alisisitiza kuwa njia ya kidiplomasia ndiyo njia pekee ya kuondokana na mvutano juu ya peninsula ya Korea , naye alisisitiza kuzuia hatua yoyote ya kijeshi inaweza kuwa mbaya na matokeo yasiyotabirika.

Naye waziri wa ulinzi wa Marekani, James Mattis, amesisitiza kwamba bado kuna nafasi ya kidiplomasia kushughulikia suala la Korea ya Kaskazini.

Mapema , Rais Donald Trump aliweka wazi msiamamo wake kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba njia ya mazungumzo sio jibu la mzozo huo.