Mji wa Tal Afar,Iraq wakombolewa

Iraq
Image caption Tal Afar, Iraq

Vikosi vya majeshi ya serikali ya Iraq vimefanikiwa kukomboa eneo zima karibu na mji wa Tal Afar kaskazini magharibi mwa Iraq ambapo kwa muda mrefu ilikuwa ni ngome ya wanamgambo wa kiislam, IS.

Majeshi ya kawaida ya Iraq na wanamgambo wengi wa Shia ambao wanawasaidi wameelezea hali ilivyokuwa kwamba Vita kwa mji wa al-Ayadiya karibu na Tal Afar sasa imekwisha.

Wanamgambo hao wa Islamic State wametoroka katika eneo hilo na kwenda kujihifadhi sehemu zingine baada ya kukimbia mji huo wa Tal Afar.

Wanajeshi nchini Iraq wameelezea mapambano baina yao na wanamgambo wa IS kuwa yalikuwa makali kuliko ilivyokuwa katika mji wa Mosul.