Iraq imetangaza kuokoa jimbo la Nineveh mikononi mwa IS

Mapigano ya Ayadiya yalichukua muda mfupi lakinimakali mno Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano ya Ayadiya yalichukua muda mfupi lakinimakali mno

Waziri mkuu wa Iraq amesema kuwa jimbo la Nineveh "limeokolewa kabisa" kabisa mikononi mwa kundi linalojiita Islamic State, baada ya Wilaya ya Tal Afar kurejeshwa kwa serikali.

Tangazo hilo la Haider al-Abadi, linafuatia kushindwa kwa wapiganaji hao wa jihadi katika mji wa Ayadiya, mahali ambapo wanamgambo hao walikuwa wamekimbilia baada ya kufurushwa mjini Tal Afar.

Maeneo machache mno ya mijini kwa sasa yanashikiliwa na IS pamoja na maeneo kame ya jangwani katikati na magharibi mwa Iraq.

Katika miezi ya hivi karibuni, kundi hilo la wapiganaji limepata pigo kubwa mno.

"Furaha yetu imetimia, ushindi umefika na Jimbo la Nineveh kwa ujumla uko mikononi mwa majeshi yetu," taarifa ya Waziri mkuu imesema.

Wapiganaji wa IS, wametwaa na kudhibiti eneo kubwa la jimbo la Nineveh pamoja na mji wa Mosul, uliotwaliwa mwezi Juni 2014.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lango kuu la kuingia mji wa Tal Afar, likiwa na maandishi ya kundi la Islamic State

Katika mapigano huko Ayadiya, mji mdogo ambao wapiganaji wa Islamic State walikimbilia kujinusuru, baada ya kubanduliwa kutoka Tal Afar, wanajeshi wa serikali walizidisha mashambulio mabaya ya angani pamoja na mizinga kutoka kwa vifaru ya wanajeshi wa nchi kavu kulikabili kundi hilo.

Siku ya Jumanne wiki hii, maafisa wa jeshi la Iraq waliiambia shirika la habari la Reuters kuwa, mamia ya wapiganaji waliojihami na bunduki ndefu ya kuvizia, mizinga, bunduki za rashasha na makombora yenye uwezo wa kupenya ndani ya magari yasiyolipuka kwa urahisi, walitolewa ndani ya majumba ya makaazi mijini.

Kanali Kareem al-Lami, anaelezea kuvunja kikosi cha mstari wa mbele vitani cha wanamgambo hao huko Ayadiya, ilikuwa ni kama kuingia katika "lango la Jehanum".

"Tulidhani vita katika mji wa kale wa Mosul vilikuwa vikali, lakini hii ilikuwa mbaya zaidi," alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanajeshi wa Iraqi wakishambulia ngome ya IS mjini Ayadiya

Haijajulikana iwapo kuna raia yeyote ambaye angali ndani ya mji huo wa Ayadiya, lakini Umoja wa mataifa unasema kuwa, watu 20,000 walikuwa wametoroka Wilaya ya Tal Afar kati ya Agosti 14 na 22.

Mosul ilitekwa na IS, lakini hilo halikuwa mwisho waker, kwani wanajeshi wa Iraqiwalianzisha oparesheni kali ya kuutwa mji wa Tal Afar mnamo Agosti 20, wakijumuisha jumla ya walinda usalama 50,000 kutoka kwa jeshi, wanahewa, Polisi, vikosi maalum na wapiganaji wa kuruka kwa miavuli kutoka kundi la waislamu wa kishia wa Popular Mobilisation Forces-PMF.

Wapiganaji wa IS kwa sasa, wanadhibiti maeneo mawilio pekee nchini Iraq- karibu na mji wa Hawija, kilomita 170 (maili 105) Kusini Mashariki mwa Tal Afar, na kutokea Ana hadi Al-Qaim katika bonde la mto Euphrates, Kilomita 220 kuelekea Kusini.

Mwezi uliopita, Islamic State ilipoteza udhibiti wa Mosul, baada ya mapigano makali yaliyodumu jumla ya miezi tisa, ambayo yalisababisha vifo vya maelfu ya raia na kuwafanya wengine zaidi ya 900,000 kukosa mahali pa kuishi.