Waislam kote duniani wanaadhimisha sherehe za Eid al-Adha

Mvulana mdogo akiwa amesimama katikakati ya umati wa waumini waliopiga magoti wakati wa ibada ya ya ya Eid al-Adha mjini Manila Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manila, Ufilipino : Mvulana mdogo anaonekana akiwa amesimama katika umati wa waumini katika ibada ya Eid al-Adha

Waislam kote duniani wanasherehekea sherehe za Idd al-Adha, zinazofanyika wakati wa Hija inayofanyika kila mwaka mjini Mecca.

Sherehe hiyo ambayo pia hufahamika kama sherehe ya kutoa kafara, ni moja kati ya sherehe kubwa za kiislam.

Ni kumbu kumbu ya kujitolea kwa utashi kwa Abraham kumtoa kafara mwanae kwa Mungu na wakati wa sherehe hii waislam hutoa kafara wanyama.

Soko la wanyama lenye shughuli nyingi likiwa na mamia ya watu waikagua wanyama nchini Misri , kabla ya siku ya mapumziko ya Eid al Adha Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika soko la wanyama la Ashmun cattle nchini Misri, wafanyabiashara wakiuza wanyama kwa ajili ya kafara kabla ya sherehe za Eid al Adha
Msichana akipakwa tatuu ya Henna mkono wake kwa jili ya sherehe za Idd al Adha katika jimbo la India la Kashmir Haki miliki ya picha EPA
Image caption Msicha wa kiislam katika jimbo lililojitangazia uhuru wake la Kashmir alipakwa Henna tattoo kwa ajili ya sherehe
Muislam wa Ufilipino akiwa amevalia vazi la rangi ya manjano na nyeusi kabla ya ibada Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mjini Manila, mwanamke akitazama simu yake, kabla ya kuazna kwa ibada
Kijana mdogo aliyevalia vazi la Spider-Man na kofia ya balagashia akiwatazama kondoo wakati wa Eid al-Adha Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kondoo , waliopangwa tayari kwa kutolewa kafara, wakitazamwa na muislam mjini Beijing, Uchina
Msururu wa wanawake waliovalia mavazi meupe wakati wa ibada ya Eid al Adha katika jimbo la Banda Aceh Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanawake wakihudhuria ibada katika jimbo la Bandeh Aceh, Indonesia
Mtoto aliyevalia vazi la rangi ya manjano akitizama kamera , huku makumi kadhaa ya watu waliovalia mavazi ya rangi mbali mbali wakionekana nyuma yake Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mjini Jakarta, watu wakisubiri kuanza kwa maombi katika mtaa mmoja nje ya msikiti

.

Mada zinazohusiana