Afrika kwa picha wiki hii : 25 - 31 Agosti 2017

Baadhi ya picha bora kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika na waafrika walio nje ya bara la Afrika

Haki miliki ya picha EPA

Nchini Ivory Coast mji mkuu Abidjan, watu walishiriki tamasha kwa ajili ya heshma ya watu wa jamii ya Ebrie ambao asili yao ni kutoka ufalme wa Ashanti.

Haki miliki ya picha EPA

Tamasha lililosherehekewa kwa miaka 300 katika kitongoji Abobodoume suburb marks, kikundi cha Ashanti ambacho kinafahamika zaidi katika nchi jirani ya Ghana. Lakini takriban asilimia 20 ya raia wa Ivory Coast wanajihusisha na asili ya makundi yenye uhusiano na ufalme, kulingana na shirika la habari la EPA.

Haki miliki ya picha Reuters

Alhamisi, mwanamke akiuza nguo katika soko mjini Cairo.

Haki miliki ya picha EPA

Pia nchini Misri, mwanamume ameshikilia kondoo kabla ya tamasha la kiislam la kutoa kafara la Eid al-Adha katika soko la Giza mjini nchini Misri

Haki miliki ya picha Reuters

Nchini Kenya, mwanamume mmoja akiwa amebeba mfuko mkubwa katika danguro kubwa zaidi lililoko katika mji mkuu Nairobi, kabla ya kupigwa marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini humo.

Haki miliki ya picha AFP

Kijana alijiandaa kwa pozi la jarida katika mji mkubwa zaidi nchini Nigeria wa Lagos.

Haki miliki ya picha AFP

Upigaji picha kwa ajili ya jarida linalofahamika kama jarida la Kijana Mtundu lenye lengo la kuonyesha jinsia ya uanaume, ikiwa ni pamoja kuwapiga wanaume picha wakiwa wamevalia sketi fupi

Haki miliki ya picha Reuters

Muasi wa Sudan Kusini akipigwa picha na silaha yake katika siku yake ya mapumziko eneo la Yondu karibu na mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Kaya.

Haki miliki ya picha Reuters

Waasi wakijiandaa kwa shambulio dhidi ya wanajeshi wa serikali walioko eneo la Kaya , karibu na mpaka wa Uganda

Haki miliki ya picha Reuters

Muhamiaji akimtuliza mwenzake ambaye hakuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka kituo cha mahabusu siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Haki miliki ya picha AFP

katika siku hiyo hiyo, wafuasi wa mwanaharakati Kemi Seba wakisherehekea kuachiliwa kwake nkatika mji mkuu wa Senegal Dakar, baada ya kukamatwa kwa kuchoma noti za benki za CFA.

Haki miliki ya picha Reuters

Jumamosi, raia wa Libya wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni walishindana kukimbiza farasi katika mji mkuu, Tripoli.

Mada zinazohusiana