Wafungwa wanavyofarijiwa na barua Kenya
Wafungwa wanavyofarijiwa na barua Kenya
Barua ni njia ya mawasiliano ambayo kwa miaka mingi imesaidia mamilioni ya watu kupitisha ujumbe duniani kote. Lakini ujio wa teknolojia za digitali umechukua nafasi ya sanaa hii ambayo sasa inasahaulika.
Lakini kuna watu ambao barua ndio njia pekee ya wao kuzungumza na jamaa na marafiki; wale walio jela.
Tarehe 1 Septemba ni siku ya kuandika barua kote duniani na mwanahabari wa BBC Mercy Juma anaelezea thamani ya barua kwa raia wa nchi nyingine waliofungwa jela katika gereza la Wanawake la Langata mjini Nairobi.