Korea Kaskazini yasifia jaribio jingine la nyuklia

North Korean leader Kim Jong-un in this undated photo released by North Korea's Korean Central News Agency (KCNA) in Pyongyang September 3, 2017. Haki miliki ya picha Reuters/KCNA
Image caption Kim Jong-un alipiwa picha akiwa na kile ambacho vyombo vya habari vilisema kwa liliku ni aina mpya ya bomu la hydrogen

Korea Kaskania imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia jaribio bomu la nyuklia ambalo linaweza kuwekwa kwenye kombora la masafa marefu.

Taifa hilo la koministi lilisema jaribio hilo la sita la bomu la nyuklia, lilifanikiwa saa kadhaa baada ya mitetemeko mitatu kutambuliwa.

Korea Kaskazini ilisema ililifanyia jaribio bomu la haidrojeni, kifaa ambacho kina nguvu zaidi kuliko bomu la nyuklia.

Wadadisi wanasema kuwa kuna ishara kuwa uwezo wa nyuklia wa Korea Kaskazini unazidi kukua.

Watabiri wa hali ya hewa mapema walitambua tetemeo dogo la ardhi, eneo ambapo Korea Kaskazini ilikuwa imefanyia majaribio ya nyuklia awali.

Tetemeko hilo dogo lilitokea saa kadha baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kupiwa picha akiwa na kile ambacho vyombo vya habari vilisema kwa liliku ni aina mpya ya bomu la hydrogen.

Haki miliki ya picha EPA/USGS
Image caption Korea Kaskazini ilisema kuwa tetemeo hilo la ardhi lilitokea katika kaunti ya Kilju, lilipo eneo la kufanyia majaribio ya nyuklia la Punggye-ri.

Vyombo vya habari vilisema kuwa kifaa hicho kinaweza kutundikwa kwenye kombora la masafa marefu.

Korea Kusini ilisema kuwa tetemeo hilo la ardhi lilitokea katika kaunti ya Kilju, lilipo eneo la kufanyia majaribio ya nyuklia la Punggye-ri.

Muda baadaye Rais wa Korea Kaskazini Moon Jae-in aliita mkutanao wa dharura wa baraza za lake la usalama wa taifa.

Ripoti za awali kutoka kwa idara ya hali ya hewa ya Marekani zilitaja tetemeko hilo kuw la ukubwa kwa 5.6 lakini baadaye likasema kuwa ukubwa huo ni wa 6.3 katika vipimo vya richa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamke mtangazaji maarufu zaidi nchini humo Ri Chun-hee

Mada zinazohusiana