Cyril Ramaphosa akiri kuwa na mpenzi nje ya ndoa

Cyril Ramaphosa(kushoto) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cyril Ramaphosa(kushoto)

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amekiri kuwa ana mpenzi nje ya ndoa, lakini amekana ripoti kuwa kuwa ana wapenzi kadhaa akisema kuwa hiyo ni sehemu ya jitihada za kumchafulia jina.

Bwana Ramaphosa alisema anaamini kuwa mali ya serikali ilikuwa ikitumiwa kumzuia kuwania uongozi wa chama cha African National Congress mwezi Novemba. wakati Rais Jacob Zuma atang'atuka wadhifa huo.

Mwandishi wa BBC nchini Afrika Kusini anaeleza kuwa inaonekana kuwa barua pepe za Bwana Ramaphosa, zilidukuliwa ili kuthibitisha uhusiano wa kimapenzi kati yake na daktari mmoja.

Jana Bw. Ramaphosa alijaribu na kushindwa kuzuia gazeti moja kuchapishwa taarifa hizo.

Barua pepe hizo zilisema kuwa Ramaphosa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa wanawake kadha wenye umri mdogo