Ukosefu wa maji watatiza kilimo cha mizabibu Dodoma
Huwezi kusikiliza tena

Ukosefu wa maji watatiza kilimo cha mizabibu Dodoma

Wakulima wa zabibu katika shamba la ushirika la Chambuma AMCOS, linalomilikiwa na zaidi ya wakulima 200 lililopo katika kijiji cha Chinangari, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma nchini Tanzania, hawajamwagilia maji mizabibu yao kwa miaka miwili.

Hii ni kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya umwagiliaji wa matone na kusababisha hofu ya kupungua kwa uzalishaji wa zao hilo.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga ametembelea shamba hilo na kuzungumza na Saidi Shadrack ambaye ni mmoja kati wa wakulima hao na kwanza akamuuliza mzabibu unaoteshwaje?

Mada zinazohusiana