Mwanahabari mashuhuri Gauri Lankesh auawa India

Lankesh alikuwa mashuhuri nchini India
Image caption Lankesh alikuwa mashuhuri nchini India

Mwanahabari nchini India ambaye pia ni mwanasiasa wa mrengo wa kushoto nchini humo ameuawa kwa kupigwa risasi.

Gauri Lankesh aliyekuwa akihariri gazeti la kila wiki, alikutwa katika bwawa la kuogelea nyumbani kwake mjini Bangalore,huku damu zikiwa zimetapakaa.

Image caption Wanafamilia wakiomboleza

Polisi wanasema amepigwa risasi mara mbili kichwani na watu waliovamia nyumbani kwake wakiwa na pikipiki.

Serikali imeyataja mauaji hayo kama kupunguza uhuru wa demokrasia.

Hakuna aliyekamatwa mpaka sasa.