Mbowe: Madaktari wanapigana kumuokoa Tundu Lissu Nairobi
Huwezi kusikiliza tena

Mbowe: Madaktari wanajitahidi kumuokoa Tundu Lissu Nairobi

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi Alhamisi mjini Dodoma, Nairobi anaendelea kupokea matibabu alikolazwa mjini Nairobi.

Kufikia saa 10 alasiri, madaktari walikuwa bado wanaendela na upasuaji wa zaidi ya saa 4 wakijaribu kutoa risasi 21 zilizokuwa zimemdhuru kiongozi huyo wa upinzani.

Mwandishi wetu Idris Situma amezungumza na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambaye aliongoza shughuli nzima ya kumkimbiza bwana Lissu Nairobi, na alianza kwa kumuuliza hali halisi ya mgonjwa ikoje?

Mada zinazohusiana