Picha za Afrika wiki hii: 1- 7 Septemba 2017

Baadhi ya picha zilizovutia kutoka Afrika na Waafrika wengineo mahala tofauti ulimwenguni wiki hii.

Mashabik wa mwimbaji wa Mali Sidiki Diabate wanaimba pamoja na yeye akiwatumbuiza kwenye uwanja wa Modivo Keita mjini Bamako siku ya Jumapili. Diabate, ni mtoto wa mchezaji maarufu wa kora, Toumani Dibate. Yeye pia ni mchezaji mzuri wa kora na pia ni mojawapo wa nyota wa mtindo wa mziki wa 'trap' barani Afrika. Haki miliki ya picha AFP

Mashabik wa mwimbaji wa Mali Sidiki Diabate wanaimba pamoja na yeye akiwatumbuiza kwenye uwanja wa Modivo Keita mjini Bamako siku ya Jumapili. Diabate, ni mtoto wa mchezaji maarufu wa kora, Toumani Dibate. Yeye pia ni mchezaji mzuri wa kora na pia ni mojawapo wa nyota wa mtindo wa mziki wa 'trap' barani Afrika.

Aliyeteuliwa kama Mrs Gabon anacheka anapovalishwa taji lake ambalo lilikuwa limeanguka wakati wa hafla ya urembo ya Mrs Universe siku ya jumamosi. Gwen Madiba alikuwa nambari mbili katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka huu Durban, ambayo huwa wazi kwa wanawake wenye umri wa kati ya miaka 25 na 45, na ambao wana familia. Haki miliki ya picha AFP

Aliyeteuliwa kama Mrs Gabon anacheka anapovalishwa taji lake ambalo lilikuwa limeanguka wakati wa hafla ya urembo ya Mrs Universe siku ya jumamosi. Gwen Madiba alikuwa nambari mbili katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka huu Durban, ambayo huwa wazi kwa wanawake wenye umri wa kati ya miaka 25 na 45, na ambao wana familia.

Siku hiyo hiyo, mlinzi anasimama mbele ya ikulu ya Emir wa Kano kabla ya kuanza kwa tamasha la Durbar, ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Eid kaskazini mwa Nigeria. Haki miliki ya picha Reuters

Siku hiyo hiyo, mlinzi anasimama mbele ya ikulu ya Emir wa Kano kabla ya kuanza kwa tamasha la Durbar, ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Eid kaskazini mwa Nigeria.

Siku ya Ijumaa, mkuu wa Kanisa la Coptic, Papa Tawardros II, aliongoza misa ya asubuhi katika Kanisa la St Mina huko Sydney, Australia. Nchi hiyo ni nyumbani kwa jamii ya tatu kubwa zaidi ya waumini wa Coptic nje ya Misri. Haki miliki ya picha Getty Images

Siku ya Ijumaa, mkuu wa Kanisa la Coptic, Papa Tawardros II, aliongoza misa ya asubuhi katika Kanisa la St Mina huko Sydney, Australia. Nchi hiyo ni nyumbani kwa jamii ya tatu kubwa zaidi ya waumini wa Coptic nje ya Misri.

Ijumaa hiyo hiyo, kundi la wanaume linaondoa magugu kwenye Ziwa Tana, kaskazini mwa Ethiopia. Magugu hayo aina ya 'hyacinth' yametishia maisha ya wavuvi wengi Afrika Masharik Haki miliki ya picha Reuters

Ijumaa hiyo hiyo, kundi la wanaume linaondoa magugu kwenye Ziwa Tana, kaskazini mwa Ethiopia. Magugu hayo aina ya 'hyacinth' yametishia maisha ya wavuvi wengi Afrika Mashariki.

Siku hiyo hiyo, Mkenya anaketi kwenye bango nje ya Mahakama Kuu huko Nairobi ambapo Jaji Mkuu David Maraga alitangaza kufutiliwa mbali kwa matokeo ya kura ya urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti . Majina ya barabara kwenye bango yamebadilishwa na watu wanaosherehekea uamuzi huo na kubandikwa ya mwanasheria James Orengo, ambaye alikuwa wakili wa upinzani na Jaji mkuu David Maraga. Haki miliki ya picha EPA

Siku hiyo hiyo, Mkenya anaketi kwenye bango nje ya Mahakama Kuu huko Nairobi ambapo Jaji Mkuu David Maraga alitangaza kufutiliwa mbali kwa matokeo ya kura ya urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti . Majina ya barabara kwenye bango yamebadilishwa na watu wanaosherehekea uamuzi huo na kubandikwa ya mwanasheria James Orengo, ambaye alikuwa wakili wa upinzani na Jaji mkuu David Maraga.

Ijumaa hiyo hiyo, kundi la wanaume linaondoa magugu kwenye Ziwa Tana, kaskazini mwa Ethiopia. Magugu hayo aina ya 'hyacinth' yametishia maisha ya wavuvi wengi Afrika Mashariki. Haki miliki ya picha AFP

Mashabiki wa kandanda nchini Misri wanasherehekea baada ya timu yao ya taifa kuilaza Uganda 1-0 katika mechi za kufuzu kwa kombe 2018, la dunia siku ya Jumanne.

Ammo Aziza Baroud, raia wa Uholanzi, aliyeteuliwa balozi mpya wa Chad , anatoa hati ya uaminifu - waraka ambao unathibitisha uteuzi wa balozi - kwa Mfalme Willem-Alexander katika ikulu ya Noordeinde huko Hague, Jumatano. Haki miliki ya picha AFP

Ammo Aziza Baroud, raia wa Uholanzi, aliyeteuliwa balozi mpya wa Chad, anatoa hati ya uaminifu - waraka ambao unathibitisha uteuzi wa balozi - kwa Mfalme Willem-Alexander katika ikulu ya Noordeinde huko Hague, Jumatano.

Afisa wa usalama wa Cameroon wakati wa kuachiliwa kwa wanaharakati wa Anglophone kutoka jela katika mji mkuu wa Yaoundé, Cameroon, siku ya Ijumaa. Rais Paul Biya aliamuru baadhi ya wanaharakati kuachiliwa lakini haijulikani wangapi walibaki jela wala ni wangapi wanaozuiliwa bila kushtakiwa. Haki miliki ya picha Reuters

Afisa wa usalama wa Cameroon wakati wa kuachiliwa kwa wanaharakati wa Anglophone kutoka jela katika mji mkuu wa Yaoundé, Cameroon, siku ya Ijumaa. Rais Paul Biya aliamuru baadhi ya wanaharakati kuachiliwa lakini haijulikani wangapi walibaki jela wala ni wangapi wanaozuiliwa bila kushtakiwa.

Siku ya Jumapili, mtu anasafisha kaburi la Mobutu Sese Seko katika mji mkuu wa Morocco, Rabat. Kiongozi huyo aliyejukikana kama "Mfalme wa Zaire", ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alifariki baada ya kuugua saratani miaka 20 iliyopita. Sherehe ya makumbusho ilifanyika mjini siku ya Alhamisi. Haki miliki ya picha AFP

Siku ya Jumapili, mtu anasafisha kaburi la Mobutu Sese Seko katika mji mkuu wa Morocco, Rabat. Kiongozi huyo aliyejukikana kama "Mfalme wa Zaire", ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alifariki baada ya kuugua saratani miaka 20 iliyopita. Sherehe ya makumbusho ilifanyika mjini siku ya Alhamisi.

Picha ni kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images na Reuters

Kuhusu BBC