Teknolojia 'inayowatambua' wapenzi wa jinsia moja

Uso Haki miliki ya picha Stanford University

Utafiti ambao unafanyia majaribio teknolojia inayodaiwa kuwa na uwezo wa kutofautisha watu wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja umezua mzozo mkali kati ya waliotayarisha teknolojia hiyo na watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani wanadai kwamba wameunda programu ya kompyuta ambayo inaweza kuangalia uso wa mtu na maumbile yake na kutofautisha kati ya wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wengine.

Programu hiyo inaweza kutambua mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyabaini, wanasema.

Lakini watetezi wa haki za mashoga wameshutumu utafiti huo na kusema ni "hatari" na "sayansi isiyo na manufaa".

Lakini wanasayansi wanaohusika wamesema wanaopinga programu hiyo hawajaielewa vyema.

Maelezo ya kina kuhusu mradi huo yatachapishwa katika jarida moja kuhusu sifa za watu na saikolojia ya kijamii.

Kuangalia utaya

Katika utafiti huo, wataalamu waliunda programu kwa kutumia picha za wanaume 14,000 wazungu kutoka kwa tovuti ya kutafuta wapenzi.

Walitumia picha kati ya moja na tano za kila mtu na kurekodi msimamo wa mtu kimapenzi kama alivyojitangaza katika tovuti hiyo ya kuchumbiana.

Wataalamu hao wanasema programu waliyoiunda ilionekana kuwa na uwezo wa kuwatofautisha wanaume na wanawake wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja.

Katika jaribio moja, programu hiyo ilipopatiwa picha mbili ambapo moja ilikuwa na basha na nyingine ya mwanamume wa kawaida, ilifanikiwa kuwatofautisha mara asilimia 81.

Kwa wanawake, ilifanikiwa asilimia 71.

"Wapenzi wa jinsia moja huonekana kufanana. Wanaume wapenzi wa jinsia moja huwa wana jaya jembamba na pua ndefu, nao wanawake wapenzi wa jinsia moja wana taya kubwa," wanasema watafiti hao.

Lakini wakati mwingine, programu hiyo haikufanikiwa sana, mfano wakati wa majaribio mengine ilipopewa picha za wanaume mabasha 70 na wanaume 930 wapenzi wa kawaida.

Ilipotakiwa kuwachagua wanaume 100 ambao wana uwezekano mkubwa wa kuwa mabasha, iliwakosa 23.

Image caption Watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja wanahofia huenda ikatumiwa katika kamera za kisiri (CCTV) za kufanya upelelezi

Gazeti la Economist ambalo lilikuwa la kwanza kuchapisha utafiti huo limesema miongoni mwa upungufu wa programu hiyo ni kwamba imeangazia zaidi Wazungu na pia imetumia picha kutoka kwa mitandao ya kuchumbiana, ambazo mara nyingi huwa zinaashiria msimamo wa watu.

Mashirika mawili ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja yametoa taarifa kushutumu utafiti huo na kusema kwamba unaweza kutumiwa kuwadhuru wapenzi wa jinsia moja.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii