Vilipuzi viliyovtegwa Myanmar vyawajeruhi watu wa Rohingya

Azizu Haque in Bangladesh hospital
Maelezo ya picha,

Mtoto wa kiume wa miaka 15 anayetibiwa huko Bangladesh alipoteza miguu yote miwili

BBC imefanya mazungua na waislamu wa Rohingya waliojeruhiwa baada ya kukanyaga milipuko walipokuwa wakiikimbia Myanmar.

Mtoto wa kiume wa miaka 15 anayetibiwa huko Bangladesh alipoteza miguu yote miwili huku mwanamke mwingine kwenye hospitali hiyo hiyo akisema kuwa alikanyaga kilipuzi baada ya kufyatuliwa risasi.

Eneo hilo liliondolewea vilipuzi miaka ya 1990 lakini taarifa zinasema kuwa Myanmar iliweka vilipuzi vipya, madai yanayokatailiwa na Mynmar.

Zaidi ya watu 300,000 wa jamii ya Rohingya wamekimbia oparesheni mbaya ya kijeshi nchini Myanmar.

Siku ya Jumatau mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Raad al-Hussein, alisema kuwa oparesheni mbaya ya kijeshi inafanyika akiitaja kuwa mauaji ya kikabila.

Maelezo ya picha,

Sabequr Nahar alipoteza miguu yote miwili

Rohingya ambayo ni jamii isiyo na utaifa wowote, wakiwa ni waislamu wachache, wamekumbwa na mateso ya miaka mingi nchini mynmar, ambayo inasema kuwa wao ni wahamiaju haramu.

Waziri mkuu wa Bangladesh Sheik Hasina, anatarajiwa kuzuru moja wa kambi za wakimbizi nchini humo walio Rohingya.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Zaidi ya watu 300,000 wa jamii ya Rohingya wamekimbia oparesheni mbaya ya kijeshi nchini Myanmar

Alisema kuwa Myanhama ni lazima itatue shida ambazo imejiletea yenyewe.

Ikulu ya White Hosue nchini Marekani imeitaka Myanmar kuheshimu sheria na kuacha kuwahamisha raia.