Bunge limefunguliwa Kenya, upinzani umesusia

Rais Kenyatta akifungua bunge

Chanzo cha picha, KTN

Maelezo ya picha,

Rais Kenyatta akifungua bunge

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka wabunge kuheshimu katiba wakati wa kufunguliwa bunge kwenye kikao chake cha kwanza tangu ufanyike uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.

Rais Kenyatta alisema kuwa kipindi hiki ambacho Kenya inasubiri kurudiwa kwa uchaguzi uliofutwa na mahakana, ni muhumu kwa katiba kuheshimiwa.

Alirejelea matamshi yake kuwa hakubaliani na uamuzi wa mahakama ya juu wa mwezi uliopitawa kufuta matokeo ya urais, lakini alikubali kwa sababu anaheshimu katiba.

Lakini Kenyatta alisema kuwa hadi pale rais mpya ataapishwa yeye bado ni rais.

Wabunge kutoka muungano upanzani Nasa hawakuwa bungeni kwa sababu wanapinga kikao hicho wakisema kuwa bado nchi inasubiri kufanya marudio ya uchaguzi.

Wakati wa kufunguliwa kwa bunge NASA nao walikuwa wakiendelea na mkutano wao katika ngome yao kisiasa, mtaa wa Kibera mjini Nairobi.

Bunge linafunguliwa huku wakenya wakijiandaa tena kupiga kura tarehe 17 mwezi Oktoba.

Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya iliamrisha uchaguzi wa urais kurudiwa kutoka na hitilafu zilizotokea kwenye uchaguzi mkun uliofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.