Jengo la mfanyabiashara tajiri kuuzwa Rwanda

Jengo la mfanyabiashara tajiri kuuzwa Rwanda
Maelezo ya picha,

Jengo la mfanyabiashara tajiri kuuzwa Rwanda

Serikali ya Rwanda imetangaza kupiga mnada jengo la kibiashara ambalo ni mali ya mmoja wa matajiri wakubwa wa nchi hiyo Tribert Rujugiro,ambaye sasa anaishi uhamishoni.

Kwa mjibu wa Mamlaka ya mapato ya Rwanda, Rujugiro anadaiwa kukwepa kulipa kodi ya mabilioni ya pesa.

Mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa wakati mmoja mshirika mkubwa wa chama tawala RPF alikosana na Rais Kagame.

Duru kutoka Mamlaka ya mapato zinasema kwamba Rujugiro anadaiwa malimbikizo ya kodi ya miaka 6 na faini yake kwanzia mwaka 2007 hadi 2013 ambayo ni kiasi cha dolla milioni 1,3 za Marekani.

Maelezo ya picha,

Jengo la mfanyabiashara tajiri kuuzwa Rwanda

Mwezi wa tatu mwaka huu,mamlaka ya mapato ya Rwanda iliweka jengo hilo la "Union Trade Center'' kwenye orodha ya mali 14 zilizopigwa tanji na serikali kutokana na malimbikizo ya kodi.

Kuna maduka yasiyopungua 100 ndani ya jengo hilo.wengi miongoni mwa walikuwa wanafanyia biashara zao ndani ya jengo hilo wamekwishahama na maduka mengi yamefungwa.

Wengi hawakupenda kuzungumza na BBC ,lakini mmoja miongoni mwa waliobaki amesema kwamba walipewa muda wa kujitayarisha kuhamishia biashara zao kwengineko lakini kwamba hii ni kuwaudhi wateja wao:

Maelezo ya picha,

Jengo la mfanyabiashara tajiri kuuzwa Rwanda

''Ni kweli tulisikia taarifa ya kupiga mnada jengo hili lakini sisi hatuna la kufanya kuhusu uamuzi huo.tulifahamishwa kwamba tunapashwa kuhama miezi mitatu iliyopita.tulisubiri kukamilisha muda tuliopewa na ndiyo sasa umekamilika; kwa hiyo kulingana na mkataba wetu hatuna hasara yoyote ila tunaathirika kwa njia moja ama nyingine kwa sababu wateja wetu walikuwa wamezoeya hapa.Kwa hiyo kuelezea wateja kwamba tumehamisha huduma kwengineko ni kama kuwaudhi.''

Mwaka 2014 Bunge la Rwanda lilipitisha sheria inayohusu serikali kudhibiti mali ya raia wa Rwanda ambao hawaishi nchini humo.

Maelezo ya picha,

Jengo la mfanyabiashara tajiri kuuzwa Rwanda

Wakosoaji wa serikali hata hivyo walisema kuwa ni njama ya serikali kuchukua mali ya watu wanaoonekana kuwa wapinzani wake.Miongoni mwa mali hizo zilizopigwa tanji ni jengo hilo la Union Trade Center.

Mmiliki wake Tribert Rujugiro sasa yuko uhamishoni baada ya kuwa mshirika mkubwa wa chama tawala RPF kwa miaka kadhaa kabla ya kuhama nchi hiyo.

Tarehe ya mnada wa jengo hilo iliyotangazwa ni 25 mwezi huu.