Chuo kikuu cha Makerere chachunguza shahada bandia

Chuo kikuu cha Makerere Uganda

Chanzo cha picha, Makerere University

Maelezo ya picha,

Chuo kikuu cha Makerere Uganda

Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kinachunguza uhakiki wa alama na viwango vya shahada zilizotolewa tangu 2011 kwa lengo la kuziangazia upya zile zilizotolewa kinyume na sheria

Chuo hicho ambacho kimewezaa wanasiasa kama Vile Julius Nyerere na Milton Obote kimeamua kuziangazia shahada zake ambazo zilitolewa kinyume na sheria baada ya kubaini tofauti kati ya matokeo yaliotolewa na chuo hicho na yale ya daraja la mwisho.

Kulingana na gazeti hilo,chuo hicho kimesema kuwa ''waziri mmoja wa zamani pamoja na wabunge kadhaa wataathiriwa''.

Gazeti hilo limewanukuu maafisa wa polisi wa Uganda wakisema kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho ambao hawakumaliza masomo walighushi vyeti bandia ambazo hutumia kama vyeti rasmi.

Ufichuzi huo umesababisha kusimamishwa kazi kwa maafisa sita ambao wanawasaidia polisi kwa uchunguzi.

Wiki kadhaa baada ya sherehe ya kufuzu kwa mahafala mnamo mwezi Machi , chuo hicho kilifunga mfumo wa kutoa matokeo wa mtandaoni na kusimamisha utoaji wa matokeo.

Kulingana na gazeti la The Monitor, mfumo huo wa matokeo ya mtandao ulikuwa ukitumiwa kuhifadhi matokeo ya wanafunzi.

''Tumeamua kuchunguza matokeo ya miaka mitano iliopita,alisema naibu kansela wa chuo hicho Profesa Barnabas Nawangwe. Akingezea kuwa watadanya uchunguzi huo kwa kina kwa kuwa vyo vyote vimeathiriwa na kwamba wataendelea na uchunguzi huo iapo mtu yeyote atashukiwa kufanya udanganyifu''.