DNA: Mjomba si baba wa mtoto wa msichana wa miaka 10 India

An image depicting child abuse

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha,

DNA: Mjomba si baba wa mtoto wa msichana wa miaka 10 India

Polisi nchini India wameanzisha upya kesi ya mtoto msichana wa miaka 10 baada ya DNA ya mtoto wake kutofautiana na ya mjomba wake ambaye ameshtakiwa kwa kumbaka.

Baada ya mahakama kuu kumnyima kibaliacha kutoa mimba, msichana huyo alijifungua mtoto mwezi uliopita.

Msichana huyo wa miaka kumi hakufahamu kuwa alikuwa mjamzito, aliambiwa kuwa tumbo lake kubwa lilitokana na jiwe lililokuwa ndani ya tumbo lake.

Anadai kuwa alibakwa na mjomba wake mara kadha kwa kipindi cha miezi saba iliyopita.

Mwanamume huyo ambaye ana umri wa takriban miaka 40 alikamatwa na ameshtakiwa katika mahakama maalum inayoshughulia kesi zinazohusu dhuluma dhidi za watoto. Bado yuko gerezani na hajasema lolote.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

DNA: Mjomba si baba wa mtoto wa msichana wa miaka 10 India

Mwandishii wa BBC mjini Delhi anasema kwa matokeo hayo sasa yameibua masuali ikiwa msichana huyo alikuwa amebakwa na watu wengine.

Baba yake msichana huyo alikuwa mapema ameiambia BBC kuwa mwanamume huyo hajakataa mashtaka dhidi yake, Polisi wanasema kuwa mjomba wake msichana huyo alikuwa amekubali madai hayo.

Naye mama yake msichana huyo ameripotiwa kuwaambia wachunguzi kuwa hawamshuku yeyote, kwa hivyo kesi hiyo imechukua mkondo mwingine,

Siku ya Jumanne polisi na watoa ushauri walitembelea familia hiyo tena kuzungumza na mtoto huyona msichana wa miaka 10

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

DNA: Mjomba si baba wa mtoto wa msichana wa miaka 10 India