Mashambulizi ya Marekani yawaua al-Shabab 6 Somalia

Al-Shabab wametangaza kutii kundi la al-Qaeda na wameahidi kutoa mazingira salama kwa mashambulizi ya kigaidi kote duniani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Al-Shabab wametangaza kutii kundi la al-Qaeda na wameahidi kutoa mazingira salama kwa mashambulizi ya kigaidi kote duniani

Jeshi la Marekani limesema kuwa limewaua wanachama sita wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab kwenye mashambulizi matatu ya angani kusini mwa Somalia.

Kituo cha jeshi la Marekani barani Afrika kimesema kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Somalia, jeshi la Marekani liliendesha mashambulizi matatu ya angani nchini Somalia dhidi ya kundi la al-Shabab ambapo wanamgambo 6 waliuawa.

Oparesheni hiyo ilifanyika kusini mwa Somalia karibu umbali wa kilomita 260 kusini mwa mji mkuu Mogadishu.

Al-Shabab wametangaza kutii kundi la al-Qaeda na wameahidi kutoa mazingira salama kwa mashambulizi ya kigaidi kote duniani

Pia al-shabab wametangazawazi kujitolea katika kupanga na kuendesha mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake eneo hilo.

Jeshi la Marekani linasema kuwa liitaendelea kutumia kila mbinu kuwalinda raia wake kutokana na vitishi kutoka kwa magaidi kwa lengo na kuwashambulia magaidi na kambi zao za mafunzo kote nchini Somalia na kote duniani.