Ukosefu wa umeme wasababisha watu 5 wazee kufariki Florida

Florida nursing home evacuated

Chanzo cha picha, WFOR-TV

Watu watano katika makao ya kuwatunza watu wazee ambayo yalibaki bila umeme kwa siku kadhaa baada ya kimbunga Iram wamefariki.

Polisi waliondoa karibu watu 120 kutoka makao hayo seo Jumatano baada ya makao hayo kubaki bila vifaa vya huduma za hewa.

Meya mmoja alisema kuwa watu watatu walipatikana wakiwa wamekufa katika makao ya Holltwood Hills na wawili walifariki walipofikishwa hospitalini.

Watu milioni 10 bado hawana umeme huko Florida, Georgia na Carolina baada ya kimbunga Irma.

Irma ambacho kimewaua watu kadha nchini Marekani, kilikumba kusini magharibi mwa Florida siku ya Jumapili asubuhi.

Si makao tu ya huko Florida yaliyobaki bila umeme baada ya kimbunga Irma.

Zaidi ya nusu ya makao ya watu wazee huko Pembroke Pine, Florida bado hawakuwa na umeme hadi leo Jumatano.