Majimbo ya Burma yakumbwa na vurugu

Burma

Chanzo cha picha, EPA,BBC

Maelezo ya picha,

Watu walio wengi wanaoingia Bangladesh walianza safari wiki moja iliyopita

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hali ya watu wa Rohingya Myanmar ni janga, na kuwataka wenye dhamana ya uongozi nchini Burma kusitisha vurugu katika jimbo la Rakhine .

Antonio Guterres alielezea hali ya makaazi hayo kuwa kama sehemu ya tatu ya utakaso wa kikabila kwa Rohingyas , na kuonya kuwa mgogoro huo unazidi kukua na kugeuka kuwa uharibifu wa kikanda .

Inaarifiwa kuwa mamia ya maelfu ya Waislamu wa eneo hilo la Rohingyas wamekimbilia Bangladesh , na bwana Guterres amesema hali yao ya kibinadamu ni mbaya.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limeshutumu vikali vurugu zinazoendelea katika jimbo la Rakhine , na kusema kuwa hatua za makusudi hazina budi kuchukuliwa haraka iwezekanavyo kusitisha hali hiyo.