Marekani yailaumu Kremlini kwa udukuzi

Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eugene Kaspersky ndiye muanzilishi wa programu ya Kaspersky Lab mnamo mwaka 1997

Idara ya Marekani ya Usalama wa mambo ya ndani umetoa agizo kwa idara zote za serikali na mashirika kutekeleza mipango ya kuondoa programu zote za Kaspersky Lab kutoka katika mifumo yao ya komputa.

Idara hiyo imefafanua sababu za agizo lake kuwa ni kutokana na wasiwasi kuhusu uhusiano kati ya viongozi ambao wanafanya kazi na kampuni ya Moscow na vyombo vya usalama vya Urusi .

Hatua hiyo imefikiwa huku bunge la Seneti nchini Marekani wiki hii likijiandaa kupiga kura kuzuia matumizi ya programu hiyo katika ofisi za serikali na pia bidhaa za kampuni hiyo.

Kaspersky Lab tayari imerudia kukana tuhuma dhidi yake kwamba uhusiano na Kremlin.Ingawa harakati hizo za kujitetea hazijabadili mtazamo ya wa jamii na serikali kwa ujumla na hivyo kusababisha wauzaji wengi wa Marekani kuondoa bidhaa zake sokoni.

Kaspersky ina wateja zaidi ya milioni mia nne duniani kote , lakini haijawahi kufanikiwa kuwa muuzaji mkuu kwa serikali ya Marekani.