BBC yatetea wafanyakazi wake Iran

BBC

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

BBC

Shirika la utangazaji BBC limetoa wito kwa serikali ya Iran kuzuia unyanyasaji kwa waandishi wake. Akizungumza kupitia runinga ya jamii ya kifalme ,mwenyekiti wa BBC, Sir David Clementi alizungumza juu ya wasiwasi wake kwamba mfumo wa mahakama wa Irani ulikuwa umeongeza shinikizo kwa wafanyakazi wa huduma ya Kiajemi iliyoko nchini Uingereza.

Mahakama imekuwa nyenzo ya kufungia mali ambazo bado zinashikiliwa nchini Iran. BBC imetaka wafanyakazi wake waruhusiwe kupata haki sawa za kifedha kama ilivyo kwa wananchi wake.

Inaarifiwa kuwa huduma ya Kiajemi ni marufuku nchini Iran , na pia kufanya kazi shirika la utangazaji BBC ni kinyume cha sheria. Ingawa kituo hicho kina watazamaji na wasikilizaji karibu milioni kumi na mbili unusu .