Wanafunzi 24 wafariki kwenye moto nchini Malaysia

Tahfiz Darul Quran Ittifaqiyah school in Kuala Lumpur (14 Sept 2017)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wanafunzi 24 wafariki kwenye moto nchini Malaysia

Takriban wanafunzi 24 na walimu wamefariki kwenye moto katika shule moja ya kidini kwenye mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur.

Moto huo katika shule ya Tahfiz Darul Quran Ittifaqiyah, ulitokea mapema asubuhi leo Alhamisi.

Waathiriwa wanakisiwa kukwama kwennye mabweni yao kwa kuwa madirisha yalikuwa yamefungwa na vyuma.

"Hi ni moja tu ya majanga mabaya zaidi ya moto katika kipindi cha miaka 20 iliyopita," mkurugenzi wa idara ya moto aliliambia shirika la AFP.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wanafunzi 24 wafariki kwenye moto nchini Malaysia

Taarifa za awali zilisema kuwa ziliweka idadi ya waliofaniki kuwa 25 lakini polis baadaye walisema kuwa wale waliofariki na 24.

Polisi walisema kuwa wanafunzi 22 wote wa kiumue walio kati ya miaka 13 na 17 na wafanyakazi wawili ndio walliofariki.

Watu 10 walipelekwa hospitalini na wenginen wanne waliripotiwa kuwa na majeraha mabaya.

Shule za dinia ya kiislamu ambapo watoto hujifuza Koran, wanafunzi mara nyingi huishi shuleni.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wanafunzi 24 wafariki kwenye moto nchini Malaysia

Picha na video zinazosambaa katika mitandao zilionyesha eneo lote la juu ya shule likiwa limeshika moto.

Polisi wanasena kuwa bado wanachunguza kile kilichosababisha moto huo huenda ulissbabishwa na hitilafu ya umeme au dawa ya kuchomwa ya kuzuia mbu.

Waziri wa nyumba nchini Malaysia anasema kuwa kumekuwa na visa 29 vya moto katika shule za tahfiz nchini humo tangu mwaka 2015.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wanafunzi 24 wafariki kwenye moto nchini Malaysia