Rais Robert Mugabe na mkewe Grace wajiandikisha upya kama wapiga kura

Rais Robert Mugabe akijiandikisha kama mpiga kura
Maelezo ya picha,

Rais Robert Mugabe akijiandikisha kama mpiga kura

Rais wa Zimabawe Robert Mugabe na mkewe Grace, wamekuwa watu wa kwanza kujiandikisha kama wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Rais hata hivyo alisema kuwa shughuli hiyo ya kujiandikisha ilichukua muda mrefu.

Raia wote wa Zimbabwe wakiwemo wale waliopiga kura kwenye uchaguzi uliopita, watahitaji kujiandikisha upya kwa kutumia mfumo mpya ambao unachukua alama za vidole na picha za uso.

Maelezo ya picha,

Grace Mugabe akijiandikisha kama mpiga kura

Ni vifaa 400 kati ya 3000 vya kuwandikisha wapiga kura vilivyowasilishwa nchini humo kutoka China kwa shughuli hiyo ambayo itakamilka mwezi Januari mwaka 2018.

Tume ya uchaguzi inasema kuwa inalenga kuwaandikisha watu milioni 7.

Bwana Mugabe ambaye ameingoza nchi tangu mwaka 1980, anatarajiwa kuwa mgombea wa chama cha Zanu-PF kwenye uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuandaliwa kati kati mwa mwaka ujao.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Bwana Mugabe ambaye ameingoza nchi tangu mwaka 1980, anatarajiwa kuwa mgombea wa chama cha Zanu-PF kwenye uchaguzi mwaka ujao