Tanzania: Adui wa mwanamke kiuchumi ni mwanamume?

Tanzania: Adui wa mwanamke kiuchumi ni mwanamume?

Serikali ya Tanzania inatambua kwamba kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini humo.

Wanaoathirika zaidi kutokana na kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia nchini humo ni wanawake.

Katika Haba na Haba tuko Ngara mkoani Kagera tukihoji je, adui wa mwanamke kiuchumi ni mwanamume?