Idris Sultan azungumzia fursa ya kuigiza filamu Marekani

Idris Sultan azungumzia fursa ya kuigiza filamu Marekani

Wasanii katika tasnia ya uchekeshaji waishio katika Afrika Mashariki hupata fursa ya kushiriki katika tasnia nyingine kama vile uigizaji na muziki.

Aliyekuwa mshindi wa Big Brother Afrika mwaka 2014 ambaye ni mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idris Sultan, anatarajia kushiriki katika filamu ya Kimarekani itakayoitwa 'Ballin (On the Other Side of the World),' itakayoelekezwa na Harvey White, mkurugenzi wa muziki, mhariri na mtengenezaji maarufu wa filamu nchini Marekani.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amezungumza na mchekeshaji huyo na hii hapa ni taarifa yake.