Alexis Sanchez aisaidia Arsenal kuilaza Fc Cologne

Alexis Sanchez akifunga bao la pili la Arsenal dhidi ya Fc Cologne

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Alexis Sanchez akifunga bao la pili la Arsenal dhidi ya Fc Cologne

Alexis Sanchez aliisaidia Arsenal kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Ujerumani Cologne katika mechi ya Yuropa iliocheleweshwa kwa saa moja kutokana na matatizo ya mashabiki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji bora wa mechi hiyo Alexis Sanchez wa Arsenal akisherehekea bao lake

Sanchez ambaye karibia aihame klabu hiyo ili kujiiunga na Manchester City katika siku ya mwisho ya uhamisho , aliuchukua mpira nje ya eneo hatari na kuupinda huku kipa Timo akishindwa kuokoa mkwaju huo.

Mechi hiyo hatahivyo haikuanza katika muda iliopangiwa baada ya maelfu ya mashabiki wa Cologne kuwasili katika uwanja wa Emirates bila tiketi na baadaye kuzozana na wanaowakaribisha wageni ndani ya uwanja huo.

Na mechi ilipoanza , Cologne ilichukua uongozi baada ya Jhon Cordoba kumfunga kipa David Ospina akiwa maguu 40.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mashabiki wa Cologne wakizuiwa na maafisa wa polisi katika uwanja wa Emirates

Mshambuliaji Olivier Giroud alipiga nje kichwa cha wazi akiwa maguu sita pekee karibu na goli .

Lakini mchezaji wa ziada Sead Kolasinac alisawazisha kabla ya Sanchez kufunga bao la pili.

Beki wa kulia wa Arsenal Hector baadaye alifunga bao la tatu huku kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere akiichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza tangu Agosti 2016.