Habari za Global Newsbeat 1000 15/09/2017

Habari za Global Newsbeat 1000 15/09/2017

Teknolojia ambayo huenda ikapelekea chanjo ya watoto kutolewa mara moja kwa kila mtoto imebuniwa na watafiti nchini Marekani.Chanjo hiyo itakayotolewa mara moja kwa mpigo itashirikisha dawa zote katika sindano moja ambazo zitakuwa zikifanya kazi kwa muda utakaohitajika ili kumkinga mtoto na magonjwa yanayolengwa.