Mvulana albino auawa na ubongo kutolewa Msumbiji

Chanzo cha picha, Getty Images
Mvulana wa umri wa miaka 17 ambaye ana ulemavu wa ngozi amepatikana akiwa ameuawa na ubongo wake kutolewa nchini Msumbiji.
Mkazi wa eneo la Tete, magharibi mwa Msumbiji, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema wazazi wa mvulana huyo walianza kumtafuta alipokosa kurejea nyumbani.
Mwili wake ulipatikana ukiwa hauna mikono na miguu.
Aidha, kichwa chake kilikuwa kimepasuliwa na ubongo wake kutolewa.
Msemaji wa polisi wa mkoa wa Tete Lurdes Ferreira amesema polisi wataanzisha uchunguzi eneo ambalo uhalifu huo ulitokea.
Kisa hicho ndicho cha karibuni zaidi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao mara kwa mara hushambulia kwa sababu ya viungo vyao ambavyo hudaiwa kutumiwa katika ushirikina.
Watu wenye vipara washerehekea Japan
Zaidi ya wanaume 30 wenye vipara kichwani nchini Japan wanaadhimisha siku kuu yao ya kila mwaka inayoshirikisha mchezo wa kuvuta kamba.