Tanzania: Ala za muziki za kitamaduni zinavyowafaidi Wagogo

Tanzania: Ala za muziki za kitamaduni zinavyowafaidi Wagogo

Utamaduni wa asili umekuwa ni sehemu muhimu katika jamii ya Afrika Mashariki.

Nchini Tanzania, utamaduni wa Wagogo umekuwa na alama za kipekee za kuutambulisha utamaduni wa kabila hilo kutokana na kuwepo kwa zana za kipekee za muziki wa asili kama vile Marimba na Zeze ambapo kwa baadhi ya wakazi hufanya biashara ya zana hizo kwa wenyeji na wageni katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amezunguza na wenyeji wa mkoa huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.