Hamas na Fatah kuanza majadiliano ya kuunda serikali ya muungano

This file photo taken on July 03, 2015 shows a Palestinian man waving the green flag of the Islamist movement Hamas during a demonstration outside the Dome of the Rock at the Al-Aqsa Mosque compound in Jerusalem.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Hamas na Fatah kuanza majadiliano ya kuunda serikali ya muungano

Kundi la Hamas lenye mamlaka huko Gaza, linasema linataka kuanza majadilano na wapinzani wao Fatah, ambao wana nafasi kubwa katika mamlaka inayoongozwa na rais Mahmoud Abbas huko upande wa ukingoni magharibi kwa lengo la kutaka kuunda serikali ya muungano.

Taarifa rasmi ya Hamas inasema itaanza kwa kuivunja kamati yake ya utawala wa Gaza na kisha kuitisha uchaguzi mkuu.

Hatua hiyo inafuatia mazungumzo baina ya viongozi wa Hamas na maafisa wa ngazi ya juu kutoka Misri.

Kundi la Fatah kwa upande wao wamesema wanakaribisha hatua hiyo.

Tangu mafarakano ya hapo 2007, wakati ambapo Hamas ilishinda uchaguzi wa eneo hilo, hatua mbalimbali zimechukuliwa kujaribu kupatanisha pande hizo mbili bila mafanikio. The Palestinian militant

Hamas wanatambuliwa na kundi la kigaidi na Israel, Marekani, Muungano wa nchi za Ulaya, Uingezea na mataifa mengine.

Tangu mwaka 2007 Israel na Misri wameweka vizuizi vya ardhini na hewani kwa ukanda wa Gaza kwa lenga la kuzuia mashambulizi kwa wanamgambo wa Gaza.