Aung San Suu Kyi atakiwa kukomesha mateso na mauaji yanayowakumba Rohingya

Rohingya stretch their hands to get aid supplies in Cox's Bazar, Bangladesh. Photo: 16 September 2017

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

San Suu Kyi atakiwa kukomesha mateso na mauaji yanayowakumba Rohingya

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amemtaka kiongozi wa Myanmar Bi ,Aung San Suu Kyi, kuchukua hatua za haraka kukomesha mateso na mauaji yanayowakumba waislamu wa Rohingya

Bw Guterres amesema Bi Aung San Suu Kyi ambaye anatarajiwa kuhutubia taifa lake hapo Jumanne, ana kila nafasi ya kuingilia kati kuzuia maafa hayo.

Wakati huo huo polisi wa Bangladesh wametangaza utaratibu na mipangilio inayonuiwa kufuatilia vipi wakimbizi wa jamii ya wa Rohingya watakavyohifadhiwa nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya polisi wa Bagladesh wakimbizi hao laki nne wa Rohingya waislamu, itabidi wasalie katika kambi walizotengewa, badala ya kujichanganya na raia wengine wa Bangladesh .

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

San Suu Kyi atakiwa kukomesha mateso na mauaji yanayowakumba Rohingya

Serikali ya Bangladeshi iko katika harakati za kujenga kambi kubwa kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi laki nne waliotoroka mateso Myanmar, katika kipindi cha wiki tatu pekee.

Tayari kuna maelfu ya wakimbizi wa jamii ya Rohingyas waishio Bangladesh tangu walipotoroka na madhila yanayowapata huko Myarmar.

Wadadisi wanasema, msimamo huo wa Bagladesh unanuiwa kutambulika vyema kwa wakimbizi hao ili baadae warudi makwaoMyanmar ikitumainiwa matatizo yanayowakumba yatatatuliwa haraka.

Maelezo ya picha,

San Suu Kyi atakiwa kukomesha mateso na mauaji yanayowakumba Rohingya