Hurricane Maria kuharibu zaidi Caribbean

Muonekano wa kimbunga Maria kwenye picha za satelite
Maelezo ya picha,

Muonekano wa kimbunga Maria kwenye picha za satelite

Watabiri wa hali ya hewa nchini Marekani wanasema kimbunga Maria kwa sasa kimejiimarisha na kuonekana kuelekea kupiga pande za Mashariki mwa visiwa vya Caribbean.

Maria kinatabiriwa kuongezeka nguvu zaidi na kupiga baadhi ya sehemu ambazo kimbunga Hurricane Irma kilipiga mapema mwezi huu.

Baadhi ya sehemu zinazotajwa kupigwa ni Dominica, Guadeloupe ,St Kitts na Nevis.

Maelezo ya picha,

Baadhi ya madhara ya Hurricane Irma

Irma ni miongoni mwa vimbunga vikali kuwahi kupiga bahari ya Atlantic kikiacha zaidi watu 80 wakiwa wamekufa huku kikiharibu maelfu ya makazi ya watu na mamilioni kuachwa bila ya nishati ya umeme.