Kimbunga kikali chawaua watu 8 Romania

A man walks near a car hit by a falling tree following a storm in Timisoara, western Romania. Photo: 17 September 2017

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Upepo ulifika kasi ya kilomita 100 kwa saa ulioangusha miti na kuong'oa paa za nyumba

Kimbunga chenye nguvu magharibi mwa Romania kimewaua watu wanane na kuwajeruhi karibu wengine 67, kwa mujibu mwa maafisa eneo hilo.

Wengi wa waliothiriwa walikuwa ndani na nje ya mji wa Timisoara ambapo upepo ulifika kasi ya kilomita 100 kwa saa ulioangusha miti na kuong'oa paa za nyumba.

Baadhi ya huduma za umeme na maji zimekatwa.

"Hatukuonywa kuhusu hili, ripoti ya hali ya hewa ilisema kuwa kungekwa na mvua," meya wa mji wa Timisoara Nicolae Robu aliambia runinga moja.

Huduma za dharura nchini Romania zimewashauri watu kusalia manyumbani mwao na kuzuai kwenda karibu na miti na nyaya za umeme.

Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea kaskazini kwenda Ukrain.

Maelezo ya picha,

Kimbunga kikali chawaua watu 8 Romania