Wayne Rooney apigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miaka miwili

Wayne Rooney

Chanzo cha picha, EPA

Nahodha wa zamani wa kikosi cha England Wayne Rooney amefika mahakamani na kukiri kuendesha gari akiwa mlevi.

Alikamatwa wakati polisi walisimamisha gari lake huko Wilmslow, Cheshire tarehe mosi mwezi Septemba.

Rooney 31 alipigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miaka miwili na kuamrishwa kutoa huduma ya jamii bila malipo kwa masaa 100.

Rooney pia aliamrishwa kulipa pauni 170 wakati alifika katika mahakama ya Stockport.

Mzaliwa huyo wa Liverpool alojiunga tena na klabu yake ya utotoni ya Eveton miaka 13 tangu akihame na kuelekea Manchester United.

Baba huyo wa watoto watatu ndiye anayeshikisa rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi nchini Uingereza.