Mke wa Nawaz Sharif ashinda ubunge

Kushoto ni mke wa Nawaz Sharif na kulia ni binti yao Mariam

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kushoto ni mke wa Nawaz Sharif na kulia ni binti yao Mariam

Mke wa Waziri mkuu wa Pakistan aliyeondolewa Madarakani Nawaz Sharif, ameshinda katika kuwania kiti cha ubunge kilichoachwa na mumewe kwenye uchaguzi uliofanyika Lahore, jimbo mbalo ni ngome ya familia yao.

Matokeo yasiyo rasmi yanaonesha kuwa Kulsoom Nawaz amemshinda mpinzani wake, lakini kwa wingi mchache.

Kura hizo zInaonesha kama ni jaribio la kumuunga mkono kiongozi wa chama cha Pakistan Muslim League Nawaz Sharif, wakati kukikaribia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Waziri mkuu huyo wa zamani alienguliwa nafasi yake hiyo na mahakama kuu nchini humo mwezi Julai, kufuatia tuhuma za rushwa.

Kufuatia hali hiyo, matokeo hayo ya uchaguzi yanaweza kuonekana kama ni jambo lisilo ridhisha, kama anavyosema Alison Wood, kutoka mtandao unaojulikana kama Control Risks Group.

Kampeni za Uchaguzi huo mdogo ziliongozwa na binti yake Maryam.Hata hivyo mshindi wa kiti gicho Kulsoom Nawaz kwa sasa yuko mjini London kupata matibabu ya ugonjwa wa saratani.