Mzozo wa maji ya mto watokota baina ya Uchina na India

Mafuriko katika mto Brahmaputra

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mto hupata mafuriko makubwa wakati wa msimu wa kipupwe kila mwaka na kusababisha hasara kubwa maeneo ya kaskazini mashariki mwa India na Bangladesh

Uchina na India ziliweza kukanusha juu ya uwezekano wa mzozo wa mpaka, lakini uhasama huo unaonekana kusababisha mzozo mwingine juu ya raslimali muhimu ya maji

Serikali ya Delhi inasema kuwa bado haijapokea data za uchunguzi wowote wa kisayansi juu ya hifadhi ya maji - kwa ajili ya uchunguzi wa ugavi, mifumo wala ubora wa maji uliofanyika katika mto Brahmaputra ambao chanzo chake kiko Uchina katika kipindi hiki , kinyume na makubaliano.

Moja ya mito mikuu barani Asia Brahmaputra, unatokea eneo la Tibet na kumwaga maji yake nchini India kabla ya kuingia Bangladesh ambako huungana na vijito vidogo na kuishia Bengal.

Serikali ya Beijing imesema kuwa vituo vyake vya maji vinaboreshwa hii ikimaanisha kuwa haiwezi kushirikisha nchi nyingine taarifa zake.

Lakini BBC imebaini kuwa Uchina inaendelea kuishirikisha Bangladesh data za mto huo.

Suala la data/ taarifa za mto huo baina ya Uchina na India linakuja baada ya nchi mbili kumaliza mzozo baina yao juu ya mpaka unaozozaniwa wa Himalaya ambao ulidumu kwa zaidi ya miezi miwili.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mzozo kwenye eneo la mpaka baina ya Uchina na India umeshindwa utatuliwa kwa miaka kadhaa

Mto Brahmaputra hupata mafuriko katika kipindi cha kipupwe kila mwaka , na kusababisha hasara kubwa katika maeneo ya Kaskazini mashariki mwa India na Bangladesh.

nchi mbili zina makubaliano na Uchina yanayoitaka nchi yenye chanzo cha mto huo kushirikisha nchi nyingine data /taarifa juu ya mto huo wakati wa kipindi cha kipupwe baina ya tarehe 15 Mei na 15 Oktoba.

Kwa kawaida data hizo zinapaswa kuwa juu ya kiwango cha maji ya mto ili kutahadharisha nchi nyingine wakati wa mafuriko.

" Kwa mwaka huu... Hatujapokea data kuhusu maji ya mto kutoka kwa Uchina tangu tarehe 15 Mei hadi sasa ," alisema Raveesh Kumar msemaji wawaziri wa mambo ya nje wa India mwezi uliopita katika kikao cha kawaida cha habari.

" Hatujui sababu za kiufundi zinazosababisha haya kuna njia zilizopo za kuiwezesha Uchina kutoa taarifa za maji ya mto kwetu ."

"Mwaka jana, kutokana na haja ya ukarabati baada ya kingo za mto kuharibiwa na mafuriko na haja ya kuboresha teknolojia katika viyuo vya maji nchini India hatukuweza kukusanya data muhimu kwa sasa ," Alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina Geng Shuang katika mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita.

Maafisa kutoka Bangladesh, hata hivyo walisema bado wanapokea data kuhusu kiwango cha maji juu ya mto Brahmaputra kutoka China.

"tulipokea data za kiwango cha maji ya mto Bramahaputra kutoka China siku chache zilizopita ," Mofazzal Hossain, mjumbe wa kamati ya pamoja ya mto Bangladesh aliiambia BBC.

" Tumekuwa tukipokea data za aina hiyo kutoka kwenye vituo vitatu vya maji vuilivyopo Tibet tangu 2002 na wameendelea kutushirikisha viwango hivyo hata wakati wa msimu wa kipupwe ". Alisema Mofazzal Hossain.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mto huo hupita India kabla ya kuingia Bangladesh

Serikali ya India imeomba ipewe data kuhusu namna maji yanavyotiririka katika mto Bramahaputra katika misimu mingine , kwasababu kuna shaka nchini India kwamba Uchina inaweza kuelekeza maji ya mto huo katika majimbo yake mengine nyakati za kiangazi.

Wakazi wa Dibrugarh katika Assam, ambako mto huo ni mpana zaidi , wanasema wameshuhudia viwango maji katika mto huo vikishuka sana na kupanda sana kwa kipindi kifupi.

Kutokana na visa vya mafuriko na maporomoko ya ardhi ya mara kwa mara katika maeneo ya mto Bramahaputra uliopo karibu na milima ya Himalaya nchi zote zinahitaji data za maji ya mto huo ili kuepuka majanga hususan wakati wa msimu wa kipupwe.