Uber yawaomba radhi wateja kwa kutoa ujumbe wa ubaguzi

Uber

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Baadaye Uber ilituma ujumbe wa tweeter kwamba ujumbe huo "haukufaa kabisa".

Kampuni ya huduma za magari ya tex kwa njia ya mtandao -Uber imeomba radhi baada ya kushutumiwa kwenye mitandao ya kijamii kwa ubaguzi wa kijinsia katika ujumbe wake wa kunadi huduma zake uliotumwa kwa wateja mjini Bangalore.

Ujumbe huo uliwataka "mabwana" ku "waacha kuwapatia wake zao siku moja ya kupumzika kwa kazi za jikoni ", huku Uber ikiwaahidi kuwapa punguzo la huduma ya kuwafikishia chakula watakachoagiza kutoka kwenye maduka ya chakula.

Ujumbe huo ulisema :"Wapendwa mabwana , tunakumbusha kwamba -Leo ni Siku ya Shukrani kwa Mke ."

Baadaye Uber ilituma ujumbe wa tweeter kwamba ujumbe huo "haukufaa kabisa".

" Tumeuondoa, na tunaomba msamaha," ilisema Uber kwenye mtandao wa kijamii.

Balozi wa Uber anayesimamia mauzo, Bozoma Saint John,pia alituma ujumbe wa tweeter akisema ujumbe huo "haukukubaliki kabisa".

Ilikuwa kana kwamba watu wengi hawakuwa wameutambua ujumbe huo wa kujinadi kwa Uber au hata kuwa na hisia kinyume na ujumbe huo ," anasema mwandishi wa BBC Ayeshea Perera.

Washindani wakuu wa Uber katika huduma ya uagizaji wa chakula kwa njia ya apps nchini humo ni Zomato na Swiggy, aliongeza.

" Ikiwa Uber inataka kuendelea kuwa na soko lake thabiti itabidi iepuke kutoa ujumbe kiholela wa aina hii na kuandaa ujumbe wake kwa njia kufikirika," anasema Ayeshea Perera.

Mwaka huu Uber ilifanya uchunguzi juu ya madai ya unyanyasaji wa kingono ndani ya kampuni hiyo na kuwafuta kazi watu zaidi ya 20 kufuatia ripoti mbaya juu yao.

Kashfa hiyo ilisababisha kujiuzulu kwa wakurugenzi wakuu wa kampuni hiyo akiwemo muasisi na afisa mkuu mtendaji Travis Kalanick.

Uchunguzi huo uliendeshwa baada ya ujumbe wa blogi uliotumwa na mhandisi wa zamani wa Uber Susan J Fowler, ambao ulibaini hali ya ubaguzi wa kijisia iliyompata katika kampuni hiyo. Ujumbe huo ulisambaa mitandaoni.