Uingereza: Muendesha pikipiki jela miezi 8 baada ya kujipiga selfie barabarani

Pawel Zietowski

Chanzo cha picha, CMPG

Maelezo ya picha,

Pawel Zietowski Aliendesha kwa kasi ya kilomita 188 kwa saa, kabla ya kusimamishwa na polisi tarehe 3 Juni

Mwendesha pikipiki ambaye aliendesha pikipiki yake huku taili la mbele likinyenyuliwa kutoka ardhini na kujipiga picha ya selfie amefungwa jela miezi minane.

Pawel Zietowski pia alichukuliwa picha ya video na polisi akiwa amesimama na kuyumba yumba juu ya kiti cha nyuma cha piki piki yake.

Aliendesha kwa kasi ya kilomita 188 kwa saa, kabla ya kusimamishwa eneo la Staffordshire tarehe 3 Juni.

Akimsomea hukumu yake, Jaji Judge David Fletcher amesema kuwa picha yake "ilikuwa ya kusisimua na kuogofya".

Zietowski mwenye umri wa miaka 27- kutoka eneo la Warrington, Cheshire, nchini Uingerezas aliwahi kukiri wakati mmoja kosa la kuendesha kwa hatari.

Mahakama imesema kuwa Zietowski, wa mtaa wa Higham , alikuwa akiendesha pikipiki aina ya Yamaha R6 wakati alipovutwa na maafisa wa polisi.

Aliwaambia maafisa wa polisi kwaba alikuwa anapenda sana kushiriki mashindano ya pikipiki na alikuwa akijizoweza bara barani.

Bwana Fletcher alisema kuwa alitaka video yake ichezwe mahakamani kuhakikisha Zietowski ameiona.

"ulikuwa unajionyesha kwa watu ,"alimueleza.

Jaji alimueleza kuwa saa na mahali alipoendeshea piki piki yake si sahihi kwa mazoezi anayoyasema.

Zietowski amepigwa marufuku kuendesha chombo chochote kile kwa muda wa miezi 28.