Polisi wa Misri anayewasidia wanawake wanaonyanyaswa mtandaoni

Mina Samir

Chanzo cha picha, Mina Samil

Maelezo ya picha,

Ukurasa rasmi wa Mina Samir rasmi una ufuasi wa watu takriban milioni moja

Mina Samir ana umri wa miaka 25- na ni afisa wa polisi anayefahamika sana kwa kupenda mazoezi ya mwili na viungo gym - lakini hii sio sababu inayomfanya aandikiwe maelfu ya jumbe kila wiki.

Mina samir ambaye ni maarufu kwa mazoezi ya mwili anamiliki kurasa kadhaa za mtandao wa kijamii wa Facebook akipigia debe umuhimu wa kuishi maisha ya afya na ametenga kitengo kinachozungumzia mazoezi ya mwili kwa wanawake.

Ukurasa huo unafuatwa na wanawake 800,000.

Ukurasa wake rasmi una ufuasi wa watu takriban milioni moja.

Lakini waathiriwa wa unyanyasaji wa mtandaoni walipoanza kumtumia ujumbe wakimtaka ushauri, Bwana Samir alihisi ni jukumu lake kujibu jumbe hizo.

" Muathiriwa mwanamke wa unyanyasaji mara nyingi hukabiliwa na shutuma za kutokuwa na maadili ama kutukanwa," alisema.

" Ni watu wachache ambao wanaweza kumsaidia na watekelezaji wa uhalifu huo kutumia hali hiyo kumdhalilisha zaidi ," Aliiambia Televisheni ta Misri TeN, akielezea kwamba utamaduni ambao anaamini unamkandamiza mwanamke , anataka kuwasaidia waathiriwa wa unyanyasaji huo.

Chanzo cha picha, Mina Shamir

Maelezo ya picha,

Mara kwa mara Mina Shamir hutuma ujumbe wa kuishi maisha ya afya kwenye ukurasa wake wa facebook

Maelfu ya wasichana katika jamii za mashariki ya kati, ambako imani ya mahafidhina kwamba heshima na aibu ni jambo la kawaida , wasichana hudhalilishwa wakati mwingine na watu wanaoficha utambulisho wao ambao wakati mwingine hutuma picha zao za utupu , wakitarajia kuwaondolewa umaarufu , ulibaini uchunguzi wa BBC wa mwaka 2016.

Bwana Samir amesema vita vyake dhidi ya udhalilishaji ilianza wakati msichana mmoja alipomtumia ujumbe akiomba ushauri juu ya kuzuwia rafiki yake wa kiume kutumia picha zake binafsi.

"nilimwambia kile anachopaswa kufanya na hatua anazopaswa kuzichukua. Nikaanza kupata ujumbe mwingi wa aina hiyo kila siku ," alisema afisa huyo.

" Visa vya kuwadhalilisha wanawake vimekuwa vya kutisha. Nilikuwa nikijibu ujumbe 9 ama 10 kwa siku . Sasa siwezi kumaliza kujibu ujumbe ninaoupata kwa wiki , Ninaweza kupokea maelfu ya ujumbe unaoomba msaada ."

Sifa ya Bwana Samir imeongezeka sana kiasi kwamba makundi ya Facebook ya wanawake huweka taarifa zao kwenye ukurasa wake kupata usaidizi kwa wajumbe wenye matatizo.